Thursday 12 April 2012

Changamoto Kubwa


Kuleta Sura Moja Kama ya Kwenye Qur'an

“Na ikiwa mna shaka kwa hayo Tuliyomteremshia mja wetu basi leteni Surah moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli. Na mkitofanya - na wala hamtofanya kamwe - basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe walioandaliwa hao wanaokanusha. Na wabashirie walioamini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake; kila watapopewa matunda humo, watasema: Haya ndiyo kama tuliyopewa mbele. Na wataletewa matunda yaliyofanana; na humo watakuwa na wake waliotakasika; na wao humo watadumu.”
Qur’an Sura Al- Baqara 2:23-25

Tangu kuteremshwa kwa Qur-aan, mnamo karne kumi na nne zilizopita, hakuna hata mmoja aliyeweza kuleta Surah moja yenye kufanana na yoyote iliyo ndani ya Qur-aan, kwa kufuata uzuri wake, umbuji, ubora, sheria za busara, maelezo ya kweli, ubashiri wa uhakika na sifa nyingine za ukamilifu.

Tambua kuwa, Sura ndogo kabisa ndani ya Qur’an ni Surat Alkawthar (sura ya 108) ina maneno kumi tu, lakini bado hakuna yeyote aliyemudu kuitekeleza changamoto hii, kwa wakati huo wala katika zama hizi.[1]
 Baadhi ya makafiri wa kiarabu ambao walikuwa maadui wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walithubutu kutaka kutekeleza changamoto hii ili waoneshe kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa mtume wa kweli, lakini walifeli.[2] Kufeli huku kulitokea licha ya kuwa Qur’an iliteremshwa katika lugha yao na kwamba, Waarabu katika zama za uhai wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa waimbaji sana ambao walikuwa wakitunga Hadiyth na mashairi bora, ambayo yangali yanasomwa na kutambulika mpaka katika zama hizi lakini hawakuweza kuandika kuifikia Qur’an.
__
[1] Angalia Al-Burhaan fiy ‘Uluum Al-Qur-aan, Al-Zarkashy, juz.2. uk. 224
[2] Angalia Al-Burhaan fiy ‘Uluum Al-Qur-aan, Al-Zarkashy, juz.2. uk. 226

No comments:

Post a Comment

Qur'an 5:32